Mwanamke Amekutwa Amekufa Huku Nyoka Mwenye Sumu Aliyemfuga akiwa Amemzunguka Kwenye Shingo
#Mwanamke mmoja amekutwa amekufa katika jimbo la Indiana nchini Marekani ahuku nyoka mwenye sumu akiwa amemzunguka katika shingo.
#Laura Hurst ambaye alikuwa na umri wa miaka 36, alikutwa maiti na polisi mara baada ya kufika katika mji wa Oxford.
#Nyumba hiyo ilikuwa na nyoka 140 ndani, jambo ambalo inaaminika kuwa nyumba hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kuhifadhi wanyama.
#Nyoka wapatao 20 wanamilikiwa na bi Hurst ambaye alikuwa anawatembelea mara mbili kwa wiki.
#Ingawa nyumba hiyo inadaiwa kuwa inamilikiwa na mkuu wa polisi katika kaunti ya Benton, Don Munson ambaye anaishi nyumba jirani.
#Anasema kuwa alimkuta Hurst kwenye sakafu, gazeti la nchini humo linaripoti.
#Aliliambia gazeti hilo kuwa kifo cha bi Hurst kilikuwa ni “ajali kubwa na amekuwa akionyesha ushirikiano na kila mtu”.
#Kamanda polisi katika jimbo la Indiana, Kim Riley anasema kuwa mtu huyo ambaye alimkuta Hurst aliweza kuwaondoa nyoka hao shingoni lakini watu wa dharura walipofika walishindwa kumuokoa.
#Bi.Hurst, alijeruhiwa na nyoka hao ingawa ni kitu ambacho alikuwa anakifanya kila wakati bila kudhurika.
Post a Comment
Post a Comment